FIKRA KUBWA GROUP
FIKRA KUBWA GROUP (21)
KIDATO CHA PILI 2016
MABIBO SEKONDARI
MABIBO SEKONDARI
Na MwL Japhet E. Moshi
Fikra Kubwa (Great Thinkers) Ni group lenye jumla ya wanafunzi 21 ninao walea shuleni kitaaluma kama mlezi wao ni wanafunzi wenye ndoto kubwa kitaaluma. Hivyo kazi yetu wazazi/walezi na wadau wote ni kuwasimamia kwa ulezi uliotukuka ili waweze kufikia malengo yao ya kufika elimu ya juu.
Group Hili ni mahali muafaka wa kupeana mikakati bora ya malezi na kitaaluma ili kuweza kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wetu wa GROUP LA FIKRA KUBWA na MABIBO SS kwa ujumla.
Katika group hili tutashirikishana mambo mbali mbali yatakayofanyika kila siku kwenye group la Fikra Kubwa na kutoka kwa walezi wengine kutoka Mabibo sekondari.
Raisi wa Afrika ya Kusini hayati Nelsoni Mandela mwaka 1991 alipata kusema
``Ni kupitia Elimu ambapo binti wa mkulima masikini anaweza kuja kuwa daktari mkubwa, na ni kupitia Elimu ambapo mtoto wa kibarua mgodini anaweza kuja kumiliki Mgodi mkubwa wa dhahabu, na pia ni kupitia Elimu hiyo hiyo ambapo mtoto wa kibarua wa shambani anaweza kuja kuwa raisi wa taifa kubwa" mwisho wa kunukuu.

Hayati Mandela alikuwa anaonesha thamani ya elimu ndio maana alipata kusema kuwa
`` Elimu iliyojitosheleza ni injini ya maendeleo, lakini elimu isiyojitosheleza ni Umasikini mkubwa"
`` Elimu iliyojitosheleza ni injini ya maendeleo, lakini elimu isiyojitosheleza ni Umasikini mkubwa"
Sisi FIKRA KUBWA GROUP (21) Tunaamini kuwa, Mwanafunzi mzuri kitaaluma hazuki tu, bali huandaliwa kutoka mikononi mwa walimu na wazazi/walezi makini.
Hivyo nitumie Fursa hii kuwakaribisha wadau wote wa FIKRA KUBWA ili tuweze kubadilishana namna mbali mbali ya ulezi na kubadilishana uzoefu wa kuwasimamia wanafunzi ili kuhakikisha wanafaulu vizuri na mwisho waweze kufika Chuo kikuu na kuondoa dhana ya kuishia kidato cha nne wakiwa wamefanya vibaya katika matokeo yao ya mtihani wa mwisho.
Imendaliwa na
Mwl Japhet E Moshi
Mlezi FIKRA KUBWA GROUP
MABIBO SEKONDARI
Mwl Japhet E Moshi
Mlezi FIKRA KUBWA GROUP
MABIBO SEKONDARI
No comments:
Post a Comment