Wednesday, 31 August 2016

IFAHAMU MIKAKATI 11 YA KUONGEZA UFAULU IDARA YA ELIMU - WILAYA YA KINONDONI.

IFAHAMU MIKAKATI 11 YA KUONGEZA UFAULU IDARA YA ELIMU - WILAYA YA KINONDONI.

Mikakati hii 11 ni mikakati ya Manispaa ya Kinondoni ya idara ya elimu ya Kuongeza ufaulu wa Kidato cha pili na kidato cha nne, mikakati hii ya idara ya elimu ilianzishwa na Afisa Elimu wetu Ndugu ROGERS SHEMWELEKWA na tuliiafiki kwa pamoja na ilipitishwa na kikao cha wakuu wa shule zote na walimu wa Taaluma mwaka jana 2015. Malezi tunayoyafanya leo hii kupitia makundi mbalimbali mashuleni kwetu ni zao la Mkakati Na. 7 kati ya 11 wa Manispaaa ya Kinondoni idara ya Elimu.

MIKAKATI 11 YA KUONGEZA UFAULU WA KIDATO CHA PILI NA NNE ILIYOPITISHWA NA KIKAO CHA WAKUU WA SHULE, WALIMU WA TAALUMA NA IDARA YA ELIMU WILAYA YA KINONDONI

1. Madarasa ya Mtihani yaani kidato cha Pili na Nne kila siku asubuhi wafanye mazoezi ya asubuhi (morning test) kwa topiki 2 kwa kila somo kwa kuanza na “syllabus” ya kidato cha I, ije cha Pili, Tatu na Hatimae kidato cha nne.

2. Mada ambazo watakuwa wanafunzi wamefanya vibaya kwa majaribio ya asubuhi, zirudiwe kufundishwa ili kujenga uelewa mzuri wa mada kwa wanafunzi.

3. Kila mwezi kufanyike majaribio ya mwezi kwa kuwa mwezi una wiki 4, kila wiki kufanyike majaribio ya Masomo 2 (Monthly Test) mwezi ukiisha masomo 8 ya Msingi yatakuwa yamefikiwa. Aidha kwa yale masomo mengine (Optional Subject) Majaribio yafanyike siku za ijumaa. Wajumbe waliazimia majaribio ya mwezi yafanyike kwa siku za jumamosi.

4. Maswali yanayotungwa yawe kwenye mfumo wa Baraza la mtihani la taifa (NECTA) ili kuwaandaa vema wanafunzi na mitihani ya taifa.

5. Kila mwanafunzi awe na daftari 2 za kila somo, Daftari la nukuu za somo (Lesson Notes) na daftari la Mazoezi ya somo hilo.

6. Ratiba ya mazoezi ya asubuhi (Morning Test) na majaribio ya mwezi (Monthly Test) ibandikwe kwenye mbao za matangazo za shule. Wazazi wa kutwa wajulishwe na walimu washirikishwe kikamilifu.

7. Ufanyike mgawanyo sawa wa wanafunzi wa kidato cha pili na nne kwa walimu wote waliopo shule ili kufanya kwa ukaribu ufuatiliaji wa maendeleo ya kitaaluma, na nidhamu za wanafunzi na kuwa mshauri wa mwanafunzi husika na kumjulisha mkuu wa shule au mwalimu mwandamizi wa taaluma juu ya mwenendo na maendeleo ya mwanafunzi. (mfano wnafunzi wa kidato cha nne wako 200 na shule ina walimu 40, ina maana kila mwalimu atalea wanafunzi 5.

8. Kufanyike ufuatiliaji wa karibu wa Nidhamu za wanafunzi na mienendo yao. Aidha walimu tuendelee kuwa wazazi na walezi bora wa wanafunzi kimaadili na kinidhamu.

9. Kila siku kuwe na ripoti ya ufundishaji na taarifa itolewe kwa mkuu wa shule. Aidha kila ijumaa kufanyike kikao cha Taaluma ambacho Mwenyekiti wake amependekezwa jkuwa Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma na Katibu Mwallimuu wa Zamu kwa wiki husika. Kwa shule zenye Makamu wa wakuu wa shule Taaluma, hawa wawe wenyeviti na katibu awe Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma. Wajumbe wawe wakuu wote wa idara za Masomo. Taarifa ya ufundishaji ya wiki iwasilishwe kwa Mkuu wa Shule.

10. Kila siku ya ijumaa Mkuu wa shule apitie taarifa zote za ufundishaji yaani class Journals, Lesson Plan, Record Keeping book (Daftari linalotunza alama za wanafunzi za mazoezi na majaribio), Subject Log book na daftari za mazoezi ya wanafunzi. Pia Mkuu wa shule afuatilie nukuu za somo zinazotolewa kwa wanafunzi (lesson Notes).

11. Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma apunguziwe vipindi ili aweze kufanya ufuatiliaji wa ufundishaji wa walimu na kila au kabla ya tarehe 05 ya kila mwezi walimu wote wafanye kikao kupitia ufundishaji wa mwezi husika. Mwenyekiti atakuwa Mkuu wa Shule na Katibu atakuwa Mwalimu Mwandamizi Taaluma. Mukthtasari wa kikao hicho utawasilishwa kwa Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa. Ni vizuri kupitia ufundishaji wa kila somo, mazoezi ya kila siku yaliyotolewa, majaribio na hali ya ufundishaji. Aidha kikao kiliamua mada kwa madarasa ya mtihani ziwe zimekwisha kabla ya mwezi Julai, 2015.

Hii ndio mikakati 11 ya kuongeza ufaulu na ni kupitia mikakati hii ambapo Mkakati Na 7 na Na. 8 wa Malezi umetupa fursa hii ya kuwa na Makundi mbali mbali ili kufuatilia kwa ukaribu maendeleo yao kitaaluma.

WITO
Wito wangu kwa walimu nchini karibuni sana Kinondoni Manispaa IDARA YA Elimu Sekondari, Karibuni Fikra Kubwa Group Mabibo mje kujifunza, na shule kama Gogoni, Bunju , Maramba Mawili mjifunze kuongeza kiwango cha ufaulu kupitia malezi kwa wanafunzi wetu.

Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
MLEZI FIKRA KUBWA GROUP.

http://fikrakubwa.blogspot.com/

https://www.facebook.com/groups/1730512107203946/

Nakala kwa
Mwl Cleopa E. SOi na walezi wote waione.

6 comments: