UTEKELEZAJI WA MIKAKATI YA D.E.O. MANISPAA YA KINONDONI NDUGU ROGERS SHEMWELEKWA ILI KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU.
DEO wetu wa Manispaa ya Kinondoni alituagiza tuweke mikakati ya kuwasaidia Watoto wetu wenye HATI MBAYA.
DEO alisema tutafute wataalamu wa MWANDIKO toka shule za msingi zilizotuzunguka ili kukomesha tatizo hili linachangia Ushukaji wa Taalamu Tanzania.
KIBWEHERI SEKONDARI;
Tumeanza kutekeleza agizo hilo wiki iliyopita kwa kuanzisha mpango maalumu wa kukomesha tatizo hilo.
Zoezi hilo tumeligawa katika awamu kuu tatu.
Awamu ya kwanza tumeanza na kidato cha kwanza.
Kisha madarasa mengine yatafuata.
Tumeanza na darasa moja kwa lengo la kupima kuna changamoto zipi zinajitokeza wakati wa utekelezaji wa mkakati.
Tukizibaini tutaboresha na kuendesha zoezi hilo kwa madarasa yote.
----------------------------------
WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MKAKATI HUU TUTAPITIA HATUA ZIFUATAZO;
1.Kuandaa vifaa,
km vile; vitabu maalumu vya JIFUNZE KUANDIKA cha darasa la kwanza.Sisi tumeanza na kimoja ambacho tumeazima Shule ya msingi Kibwegere.
Wanafunzi wameandaa; daftari maalumu la kujifunzia kuandika, penseli na kifutio n.k.
2. Kuwaandaa wanafunzi kisaikrojia.
Kabla mpango hatujaanza tulifanya yafuatao;
°°Kuzungumza na wanafunzi na kuwajuza sababu za kufeli kwao ni pamoja na HATI MBAYA.
°° Kisha wanafunzi wenyewe wakubali kuwa; wanatatizo hilo.
°°Wakishakubali, unawapa moyo kwa kuwaambia tatizo lao ni dogo saana, dawa yake ipo na watapona haraka tu.
°°Pia kuwajuza madhara ya hati mbaya na faida za hati safi. Mifano hai itumike.
°°Hapo watakuwa tayari kupata dawa ya tatizo lao bila tatizo.
3. KUANZA MAFUNZO;
Mafunzo haya yanahitaji umakini wa hali ya juu sana kwani ndio msingi wa elimu.
Sisi tumejipanga kufuata mfululizo huu;
a).Kufundisha jinsi ya kuumba herufi za msingi yaani Irabu na konsonanti. Mfano; Kikanuni ''a'' inaandikwaje na inaonekaje ikiandikwa vizuri?
b). Kupitia Uandishi wa herufi kubwa na ndogo. Mfano; ''g'' kwa herufi kubwa inaandikwaje?
c).Kuwafundisha wanafunzi kanuni za kuunga neno moja nalingine. Mfano; ''l'' na ''a''zinaunganaje?
d).Baada ya hatua hizo tatu za juu wanatakiwa wafanye mazoezi ya kutosha ya kuumba herufi.
e). Kuwaandalia matini mbalimbali zilizoandikwa kwa mkono, kisha kuwapatia wazinguchuzunge na kujifunza zaidi.
f). Kuwafundisha wanafunzi matumizi ya Alama za Kiuandishi. Mfano; matumizi ya nukta, alama ya mshangao, mkato, aya, n.k. Hatua hii ni muhimu saana.
g). Mwisho tumejipanga Kuandaa SHINDANO LA UANDISHI WA INSHA.
Zawadi mbalimbale zitatolewa ili Kuwamotisha wanafunzi na kuleta ushindani na uelewa.
Wenafunzi wakishindanishwa watafanya mazoezi mengi saana.
MASHINDANO HAYA YATAKUWA YA KUDUMU.
NB; Mkakati huo kwa sasa umeanza kuwezeshwa na Mwalimu Mzoefu na Mahiri wa somo la Kiswahili Tanzania, HAMISI AIBU.
Pia tunamshukuru saana DEO KINONDONI kwa Ufunifu wake na Kasi yake ya kufanya kazi.
MUNGU AMZIDISHIE AFYA NJEMA.
--------------------------
Wadau wa Elimu tafadhali naomba MAONI YENU. Wapi paboreshwe ili Mpango wetu uwe safi.
------------------
Imeandaliwa na;
IDARA YA KISWAHILI-KIBWEHERI SEKONDARI

No comments:
Post a Comment