OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI
SHULE YA SEKONDARI MABIBO
Barua zote zitumwe kwa Anwani ya Mkuu wa
Shule
S.L.P.90100
DAR ES SALAAM-KINONDONI
Phone:+255 754967027, +255 0655322888
Unapojibu tafadhali taja Tarehe: 04.07.2016
Kumb.
Na.KMC/ED/MSS/ GV/01
MKUU WA CHUO,
CHUO KIKUU CHA AFYA MUHIMBILI,
S.L.P.
DAR ES SALAAM.
K.K.
MWADILI WA WANACHUO,
CHUO KIKUU CHA AFYA MUHIMBILI,
S.L.P.
DAR ES SALAAM
K.K.
MKUU
WA SHULE,
SHULE YA SEKONDARI MABIBO,
S.L.P 90100
DAR ES SALAAM -KINONDONI.
Ndugu,
YAH: OMBI LA ZIARA YA WANAFUNZI 21 KIDATO CHA PILI – 2016 KIKUNDI CHA FIKRA KUBWA (GREAT THINKERS) TAREHE: 19.08.2016 SIKU YA IJUMAA.
Kichwa cha habari hapo juu chahusika.
Shule
ya Sekondari Mabibo ni ya Serikali inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni iko Kata
ya Mabibo. Wanafunzi ishirini na moja (orodha
imeambatanishwa) wa kidato cha pili wa kikundi cha Fikra kubwa, Wakiambatana na
Mwalimu wao mlezi tunaomba nafasi ya kufanya ziara ya kimasomo kwa wanafunzi wetu katika chuo
chako.
Tunaomba wanafunzi hawa watembelee Chuo /
mazingira na kuonana na uongozi wa MUHAS ili kuwatembeza katika mazingira na
kuwapa maelezo ya chuo, na hamasa ya kusoma sana kwa niaba ya Uongozi wa Chuo.
Lengo ni kuwafanya wanafunzi hawa kuwa na kiu, shauku ya
kufanya vizuri katika masomo ya sayansi na mitihani yao ili kufikia ngazi ya
Elimu ya Juu; hasa kwa hawa wenye ndoto ya kuwa madaktari badae. Kwa wao kuona na kuwepo katika mazingira ya Chuo Maarufu
chenye vitu adimu na historia athimu na kuwaona kaka na dada zao wanaosomea
mambo mbali mbali kuhusu afya ya jamii, itaongeza moyo na jitihada kubwa katika kusoma sana na kufaulu mitihani ya ngazi zote ikiwemo ya Kidato cha pili,
nne na sita hadi kufikia Chuo kikuu.
Natanguliza shukrani zetu za dhati kuridhia ombi letu na
kukutakia ufanisi mwema katika hili.
Wako katika Ujenzi wa Taifa.
JAPHET
E. MOSHI
MTAALUMA
MABIBO SEKONDARI na
MwL
Mlezi - Great Thinkers Group.
0714
781432
0755
558159
E-mail:
jeffmoshi@outlook.com
No comments:
Post a Comment