KWANINI MWALIMU AWE MLEZI KITAALUMA?
SABABU:
1.Tunalea
ili ufanyike ufuatiliaji wa karibu wa Nidhamu za wanafunzi na mienendo
yao. Aidha walimu tuendelee kuwa wazazi na walezi bora wa wanafunzi
kimaadili na kinidhamu ili kuongeza ufaulu.
2. Ni jukumu letu
kama walimu tukisaidiana na mzazi kumwandaa mwanafunzi mzuri kitaaluma.
(Fikra Kubwa Tunaamini kuwa Mwanafunzi mzuri kitaaluma hazuki tu, bali
huandaliwa). Hili jukumu la kumwandaa mwanafunzi mzuri kitaaluma
serikali imekuamini ikakupa wewe mwalimu, lifanye kwa moyo wote bila
kuangalia changamoto zinazokuzunguka kila kona.
3. Kumbuka Sisi
tulilelewa ndio maana tupo hivi tulivyo, hata nguo, viatu, magari, meza
n.k unavyoviona kuna mtu alilelewa akafikia umri wa kuweza kutengeneza
unachokiona leo. Hivyo hatuna budi kuhakikisha na sisi tunalea wanafunzi
ili kuandaa madaktari, walimu na wataalamu wengi zaidi kwa miaka
inayokuja.
4. Takwimu za ufaulu kitaifa na katika shule zetu sio
nzuri kabisa, sisi wenyewe ni mashahidi wa kwanza, ukiangalia wanafunzi
wanaosajiliwa kwa ajili ya mtihani wa taifa katika shule zetu , na
ukiangalia idadi ya wale waliochaguliwa kwenda kidato cha tano baada ya
matokeo kutoka utagundua dhahiri shairi kuwa takwimu sio nzuri kabisa.
Wanaosajiliwa ni wengi lakini wanaofaulu ni wacahche mno, hivyo
inahitajika mwalimu afanye zaidi ya jukumu lake la kufundisha ili
kubadili hizi takwimu mbaya za ufaulu.
5. Mwalimu aliwahi kuwa
mwanafunzi; hivyo mwalimu anaelewa namna gani ya kumfundisha mwanafunzi
ili afaulu kwani mwalimu yeye hakufeli. Kama mwalimu hakufeli akiamua
kumsaidia mwanafunzi kwa Moyo wa dhati huyo mwanafunzi hawezi kufeli.
Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
MLEZI FIKRA KUBWA GROUP.
http://fikrakubwa.blogspot.com/
https://www.facebook.com/groups/1730512107203946/
Nakala kwa
Mwl Cleopa E. SOi na walezi wote waione
walezi wa wanafunzi tukiwa pamoja na wanafunzi tunaowalea kitaaluma
No comments:
Post a Comment