Sunday, 4 September 2016

JINSI YA KUANDAA RATIBA YA KUSOMA KWA MWANAFUNZI UNAYEMLEA

RATIBA ZA MATUKIO YA KILA SIKU

~ Ratiba hii izingatie matukio yote ya mwanafunzi baada ya kutoka shuleni ili kumsaidia mwanafunzi kutunza muda na kumwongoza asome kulingana na muda utakao mpangia, ratiba hii izingatie muda na umbali wa mwanafunzi kutoka shule ilipo hadi nyumbani.





 RATIBA YA KUSOMA KWA MWANAFUNZI MMOJA MMOJA

~ukiacha ratiba kuu ya shule ya kila siku, wanafunzi wengi hawana ratiba binafsi za kujisomea nyumbani wenyewe, hivyo ratiba ya kujisomea inaandaliwa kwa kuzingatia masomo yaliyopo kwenye ratiba kuu ya shule, yaani somo atakalosoma leo usiku liwe ni somo ambalo kesho ataenda kufundishwa shuleni, hivyo ratiba ya kujisomea ina masomo matatu kwa siku.

MIKAKATI YA GROUP
~ inategemeana na group lenyewe mtakalounda, lakini hapa nimeweka mfano wa mikakati iliyopo fikra kubwa na jinsi ya kuitekeleza.

Orodhesha pia majina ya wanafunzi na malengo yao, pamoja na kila mmoja kila wiki atakuwa na jukumu gani mtakapokutana kwa muda wa ziada.


Mpangie kila mmoja mada aje aiwasilishe kwa wenzake, unapompangia mada ya somo husika ili aje aiwasilishe, mpe muda wakujiandaa. Lengo kupima uwezo wa mwanafunzi katika kushika na kumlazimisha mwanafunzi kusoma

Imeandaliwa na
Mwl japhet E Moshi
MLEZI FIKRA KUBWA

No comments:

Post a Comment