HATUA 10 ZA KUANZA KULEA WANAFUNZI ILI WAWEZE KUFAULU
1.
Ufanyike mgawanyo sawa wa wanafunzi wa kidato cha pili na nne kwa walimu
wote waliopo shule ili kufanya kwa ukaribu ufuatiliaji wa maendeleo ya
kitaaluma, na nidhamu za wanafunzi na kuwa mshauri wa mwanafunzi husika
na kumjulisha mkuu wa shule au mwalimu mwandamizi wa taaluma juu ya
mwenendo na maendeleo ya mwanafunzi. (mfano wnafunzi wa kidato cha nne
wako 200 na shule ina walimu 40, ina maana kila mwalimu atalea wanafunzi
5.
rejea Mkakati #7)
2. Kuwajua na kuwafahamu wanafunzi wako unaowalea.
- Ifahamu Historia ya kila mwanafunzi vizuri shuleni na nyumbani.
- Zifahamu Changamoto anazopitia kielimu na msaidie azivuke.
- Tembelea nyumbani kwake ili kumfahamu zaidi na kuonana na mzazi
kujenga conection nzuri ya kumsimamia mwanae na mwombe aridhie
kusimamamia ratiba ya kusoma ya mwanae anaporudi nyumbani..
3. Pata mawasiliano ya wazazi au walezi wake.
- Tengeneza network nzuri kati yako na wazazi kimawasiliano muda wote kwa njia ya message na ikiwezekana mpigie simu.
- Tengeneza kundi la whatsup la wazazi na walezi na wadau wa kundi
lako ili kuweza kurahisisha mawasiliano ya matukio yote yanayoendelea
kwa mwanae kila siku kwa muda wa ziada shuleni, na picha watumie waone.
4. Tengeneza jina la Group lako.
- Jina mtakalolichagua na wanafunzi wako liakisi ndoto zao na mission ya group
- Mfano Mabibo kuna magroup kama Fikra Kubwa, The winners, New
Direction, Tumaini Jipya, Good Hope, 4G, Fikra Chanya n.k lakini Ukienda
Gogoni kwa Mwl SOI wao wana NDOTO KUBWA na Yes I can. Kule Bunju kwa
Mwalimu Safina wapo MAKONDA THE WINNERS na Maramba mawili utawakuta The
white Horse.
5. Wafundishe wanafunzi wako thamani ya elimu.
-
Elimu ni ya thamani kuliko kitu kingine chochote katika taifa hili, toa
mfano wa kazi mbali mbali, mfano kulima na kusoma ipi ni kazi ngumu
n.k
Raisi wa Africa kusini Hayati Nelsoni Mandela alipata kusema kuwa
“Elimu iliyojitosheleza ni INJINI KUBWA ya maendeleo, lakini elimu isiyojitosheleza ni Umasikini Mkubwa”
“Ni kupitia Elimu ambapo mtoto wa mkulima masikini anaweza kuwa Daktari
mkubwa sana, na ni kupitia Elimu ambapo mtoto wa kibarua wa mgodini
anaweza kuja kumiliki mgodi mkubwa wa Dhahabu, na ni kupitia Elimu hiyo
hiyo ambapo mtoto wa kibarua wa shambani anaweza kuja kuwa raisi mkubwa
wa nchi”
-Tafuta watu wa kuzungumza nao kwa kuanza na wale
waliomaliza hapo shuleni waje wawasaidie wenzao wasikwame, wawaeleze
wenzao namna walivyozivuka changamoto.
- Andaa study tour nia ni kujenga hamasa zaidi ya wao kutaka kusoma ili wafaulu.
- watafutie wataalamu waliowatangulia wawafundishe hatua walizopitia
hadi wakafika walipo, Mfano: kuna anayetaka kuwa profesa, mtafute
Profesa amuelekeze, Daktari mtafutie daktari atampa mwangaza zaidi n.k
ili wakusaidie kukufundishia thamani ya elimu.
6. Wapangie kila mmoja ratiba yake ziwe ratiba mbili.
Wapangie ratiba ya matukio ya kila siku nyumbani na ratiba ya kusoma
nyumbani izingatie masomo yake ya shule siku inayofuata. Ratiba hizi
zibandikwe nyumbani mwanafunzi anaposomea na lazima awe na SAA YA
MKONONI. Ni vema akiwa anasoma awe na SAA, hii itamsaidia kuelewa muda
halisi aliosoma.
7. Wafundishe Mbinu za kufaulu na Kanuni za msingi za kuwasaidia kusoma wafaulu.
(zingatia Mbinu 30 za kufaulu mtihani toka Fikra kubwa Group)
8. Tengeneza mpango kazi na mkakati wa kundi wa siku, wiki, mwezi na miezi kadhaa.
- Siku za kuwasilisha mada kwa manafunzi mmoja mmoja.
- Siku za group discussion
- Siku watafanya test/mitihani.
- Siku watakuwa na study tour n.k
9. Usimamizi na Tathmini ( Monitoring and evaluation)
- Kama kundi halitasimamiwa vizuri, halitaweza kufanya vizuri,
usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa kundi ni muhimu saana ili kupata
matokeo mazuri ya kundi lako.
10. Chagua viongozi wa kuliongoza kundi wakati haupo, mathalani mwenyekiti na katibu wa kundi.
“Fikra Kubwa Tunaamini mwanafunzi mzuri kitaaluma hazuki tu, bali huandaliwa”.
Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
MLEZI FIKRA KUBWA GROUP.
http://fikrakubwa.blogspot.com/
https://www.facebook.com/groups/1730512107203946/
Nakala kwa
Mwl Cleopa E. SOi na walezi wote waione.
Hongereni sana kwa mikakati mizuri mliyoiweka
ReplyDelete