Wednesday, 31 August 2016

NAMNA MALEZI YA WALIMU KWA WANAFUNZI YANAVYOWEZA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU.

NAMNA MALEZI YA WALIMU KWA WANAFUNZI YANAVYOWEZA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU.

KATIKA KULEA WANAFUNZI TAMBUA CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI WAKO NA KUWASAIDIA KUZITATUA ILI WAWEZE KUFIKIA MALENGO YAO.

Unapolea wanafunzi tambua CHANGAMOTO zao wanazokutana nazo katika maisha na masomo, changamoto ambazo zinaweza kuwazuia kufikia ndoto zao na uzitatue, Hii itamsaidia mwanafunzi kufaulu vizuri.

~ Mimi nilipowatembelea wanafikra kubwa nyumbani kwao ili kutambua changamoto zilizopo shuleni na nyumbani zinazoweza mzuia mwanafikra kubwa asiweze kufikia ndoto zake, niliweza kubaini mmoja wa wanafunzi wangu nyumbani kwao hakuna umeme hivyo hawezi kusoma usiku kama ratiba niliyompangia inavyomuelekeza, baada ya kugundua changamoto hii nilimnunulia taa aina ya solar D LIGHT inayotumia mwanga wa jua ili imsaidie aweze kusoma vizuri wakati wa usiku.

Taa ile tulimkabidhi mwanafunzi huyu na alishukuru mno na kwa sasa anasoma vizuri wakati wa jioni kwani ile changamoto ya taa tuliitatua.


Hivyo nivizuri kwa mwalimu mlezi aweze kutambua changamoto za wanafunzi wake ili zisiwe kikwazo kwao kushindwa kufaulu mitihani yao.

Wanafunzi wengi wanachangamoto nyingi nyumbani na shuleni changamoto nyingi sana ambazo huwa kikwazo katika safari yao ya elimu, hivyo tusipozibaini hizo changamoto na kuzitatua mapema itakuwa nivigumu kwa mwanafunzi huyo kufaulu.

Imeandaliwa na:
MwL Japhet E Moshi
Mlezi Fikra Kubwa Group (23)
Mabibo Sekondari

No comments:

Post a Comment