HISTORIA YA KUNDI LA FIKRA KUBWA NA SAFARI YA KUTEMBELEA CHUO KIKUU CHA MUHAS
Fikra kubwa / great thinkers ni kikundi cha Wanafunzi 23 kwa sasa
wenye ndoto za kuwa madaktari bingwa cha Mabibo Sec zao la Mkakati Na.
07 wa Manispaa ya Kinondoni kati ya Mikakati 11 ya Idara ya Elimu
iliyoanzishwa na Afisa Elimu wetu Rogers Shemwelekwa tuliyoafiki Wakuu
wa Shule, Wataaluma na Walimu kuwagawa wanafunzi ktk vikundi na kuvipa
majina ya kitaaluma ambapo walimu wanapata fursa ya Malezi hasa Madarasa
ya Mtihani.
Shule yetu ya Mabibo ikiongozwa na mkuu wetu Haki
Mwasomola tuna vikundi vingi baadhi Tumaini jipya, New Direction, Fikra
chanya,nk
Gogoni sec kwa MwL Cleopa Soi kuna Ndoto kubwa na Yes I
can na Bunju sec kwa mwalimu Safina kuna Makonda The Winners ndio maana
nasema ni mkakati wa Afisa Elimu wetu Rogers Shemwelekwa kuongeza
ufaulu.
1. Mkakati wa Malezi ndio umetupa fursa hii ya kuwa chuo
adimu kwa ajili ya Wanasayansi hawa wa fikra kubwa kuona ninako
watazamia kesho wawepo.
2. Naamini wao kuona na kuwaona wanachuo
waliosoma tena nyakati ngumu elimu sio bure kama sasa na mazingira ya
kiwa magumu na bado wakafaulu itawaongezea hamasa ya kusoma kufikia
ndoto zao za kuwa madaktari.
3.Katika malezi ya fikra kubwa
tunafundisha fikra za kesho yao elimu ni injini kubwa ya maendeleo yao
na jamii, tunawaandaa kumiliki na kutawala kwa njia ya elimu,
tunawafundisha thamani ya kupenda elimu kuliko chochote, kujitambua,
kuokoa muda, kuwaonyesha thamani ya elimu.
4.Wito kwa walimu
nchini karibuni Kinondoni Manispaa idara ya elimu Karibuni mabibo
mjifunze na shule kama Gogoni, Makumbusho, Bunju mjifunze kuongeza
kiwango cha ufaulu kwa malezi.
5.Nipongeze jitihada za Rais,
Waziri wa Elimu na wadau kuona Sayansi ni masomo ya Lazima kidato cha I
-IV itasaidia Wanafunzi kuwa kama wapendavyo kama hawa wa fikra kubwa
ambao usiku na mchana naomba Mungu anisaidie nichangie sehemu kama
mwalimu wawe Madaktari wataalamubingwa kama jinsi chuo hiki watawasikia
wa fani yao na kuwaona kaka na dada zao na zaidi chuo kikuu cha afya
na tiba Muhimbili.
6.Tunaishukuru Serikali kuendeleza kutatua
changamoto za walimu wa sayansi, maabara, chemical na vitabu visififishe
ndoto zao za kuwa madaktari kwani elimu isiyojitosheleza ni umaskini
zaidi wakati inayojitosheleza kama kutoishia kidato cha nne hadi ufike
chuo kupata shahada, uzamili, uzamivu, Prof ni injini kubwa ya
maendeleo.
Wenzetu India waziri wao mkuu alitembelea Tanzania wenzetu kati ya wanachojivunia na tunu kwao ni kuwa Taifa la wanasayansi
HAYATI NELSON MANDELA alikuwa Rais wa Afrika kusini alipata kunena, "Elimu ni silaha ya kuitawala dunia"
Mwalimu akasema ili tuendelee tunahitaji pia kupambana na adui ujinga
Sisi fikra kubwa tunaamini tunaweza kuwa madaktari kwa kubadilika
tunavyofikiri tumetembelea chuo hiki tufikiri kichuo ili wajitume zaidi.
Ikumbukwe mwanafunzi mzuri kitaaluma na mtaalamu mzuri hazuki tu, bali huandaliwa.
Imeandaliwa na
Mwl JAPHET E. MOSHI
MLEZI FIKRA KUBWA GROUP
MABIBO SEKONDARI
No comments:
Post a Comment