FIKRA KUBWA GROUPZIARA YETU KUTEMBELEA CHUO KIKUU CHA SAYANSI YA TIBA YA JAMII MUHIMBILI (MUHAS) LEO.SAFARI NDIO INAANZA HAPA.
Fikra kubwa / great thinkers ni kikundi cha Wanafuhnzi wenye ndoto za kuwa madaktari bingwa cha Mabibo Sec zao la Mkakati Na. 07 wa Manispaa ya Kinondoni kati ya Mikakati 11 ya Idara ya Elimu iliyoanzishwa na Afisa Elimu wetu Rogers Shemwelekwa tuliyoafiki Wakuu wa Shule, Wataaluma na Walimu kuwagawa wanafunzi ktk vikundi na kuvipa majina ya kitaaluma ambapo walimu wanapata fursa ya Malezi hasa Madarasa ya Mtihani.
Shule yetu ya Mabibo ikiongozwa na mkuu wetu Haki Mwasomola tuna vikundi vingi baadhi Tumaini jipya, New Direction, Fikra chanya,nk
Gogoni sec kwa MwL Cleopa Soi kuna Ndoto kubwa na Yes I can na Bunju sec kwa mwalimu Safina kuna Makonda The Winners ndio maana nasema ni mkakati wa Afisa Elimu wetu Rogers Shemwelekwa kuongeza ufaulu.
Gogoni sec kwa MwL Cleopa Soi kuna Ndoto kubwa na Yes I can na Bunju sec kwa mwalimu Safina kuna Makonda The Winners ndio maana nasema ni mkakati wa Afisa Elimu wetu Rogers Shemwelekwa kuongeza ufaulu.
Mkakati wa Malezi ndio umetupa fursa hii ya kuwa chuo adimu kwa ajili ya Wanasayansi hawa wa fikra kubwa kuona ninako watazamia kesho wawepo.
Naamini wao kuona na kuwaona wanachuo waliosoma tena nyakati ngumu elimu sio bure kama sasa na mazingira ya kiwa magumu na bado wakafaulu itawaongezea hamasa ya kusoma kufikia ndoto zao za kuwa madaktari.
3.Katika malezi ya fikra kubwa tunafundisha fikra za kesho yao elimu ni injini kubwa ya maendeleo yao na jamii, tunawaandaa kumiliki na kutawala kwa njia ya elimu, tunawafundisha thamani ya kupenda elimu kuliko chochote, kujitambua, kuokoa muda, kuwaonyesha thamani ya elimu.
4.Wito kwa walimu nchini karibuni Kinondoni Manispaa idara ya elimu Karibuni mabibo mjifunze na shule kama Gogoni, Makumbusho, Bunju mjifunze kuongeza kiwango cha ufaulu kwa malezi.
5.Nipongeze jitihada za Rais, Waziri wa Elimu na wadau kuona Sayansi ni masomo ya Lazima kidato cha I -IV itasaidia Wanafunzi kuwa kama wapendavyo kama hawa wa fikra kubwa ambao usiku na mchana naomba Mungu anisaidie nichangie sehemu kama mwalimu wawe Madaktari wataalamubingwa kama jinsi chuo hiki watawasikia wa fani yao na kuwaona kaka na dada zao na zaidi chuo kikuu cha afya na tiba Muhimbili
6.Tushukuru Serikali kuendeleza kutatua changamoto za walimu wa sayansi, maabara, chemical na vitabu visififishe ndoto zao za kuwa madaktari kwani elimu isiyojitosheleza ni umaskini zaidi wakati inayojitosheleza kama kutoishia kidato cha nne hadi ufike chuo kupata shahada, uzamili, uzamivu, Prof ni injini kubwa ya maendeleo.
Wenzetu India waziri wao mkuu alitembelea Tanzania wenzetu kati ya wanachojivunia na tunu kwao ni kuwa Taifa la wanasayansi
HAYATI NELSON MANDELA alikuwa Rais wa Afrika kusini alipata kunena, "Elimu ni silaha ya kuitawala dunia"
Mwalimu akasema ili tuendelee tunahiji pia kupambana na adui ujinga
Sisi fikra kubwa tunaamini tunaweza kuwa madaktari kwa kubadilika tunavyofikiri tumetembelea chuo hiki tufikiri kichuo ili wajitume zaidi
No comments:
Post a Comment