Afisa Elimu Ndugu Rogers Shemwelekwa alipowatembelea wanakambi wa Bunju sekondari wanaojulikana kwa jina la MAKONDA THE WINNERS.
Huu ni moja wapo ya mkakati 11 ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa Manispaa ya Kinondoni ambapo Bunju sekondari kwa Mwalimu Safina amewaweka wanafunzi wake kwenye kambi moja ili waweze kujiandaa vizuri waweze kufaulu katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye mitihani.
Afisa Elimu wetu ndugu Rogers Shemwelekwa mwasisi wa mikakati hii
akiongozana na Familia yake walitembelea MAKONDA THE WINNERS na kuwapa
zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mchele na vyakula watakavyokula
pindi wawapo kambini wakijiandaa na mtihani wao wa taifa.
Wanafunzi wa kidato cha pili wa Bunju Sekondari Kikundi cha MAKONDA THE WINNERS wanafunzi anaowalea Mwalimu Safina wakiwa pamoja na Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni Ndugu Rogers Shemwelekwa alipowatembelea na familia yake.

No comments:
Post a Comment