MREJESHO
WA WAGENI WALIOALIKWA KUJA KUZUNGUMZA NA WANAFIKRA KUBWA
Na MwL MOSHI JAPHET E.
UTANGULIZI:
Tunashukuru ugeni wa Leo kutoka kwa
wanafunzi wetu wa MABIBO mwaka 2013, 2014 na 2015 Lengo la kuwakaribisha
wanafunzi hawa sita leo lilikuwa ni kuzungumza na WANAFIKRA KUBWA wawaeleze
kuwa wanatakiwa kusoma sana na kuongeza bidii katika kusoma ili wafaulu kama
wao walivyofaulu na ikibidi wawazidi kwani wao wanakila sababu ya kufaulu. IKUMBUKWE WANAFUNZI HAWA NI WALE WALIOMALIZA
HAPA MABIBO KIDATO CHA NNE MIAKA ILIYOPITA NA KISHA KUFAULU VIZURI SAANA, Hivyo
walialikwa kuja kuwasaidia wadogo zao kiushauri na kuwapa mbinu walizotumia wao
kipindi chao ili wasikwame katika safari ya kuyafikia malengo yao.Nia yetu ni
njema, kuwaambia wanafikra kubwa kuwa ELIMU ni kitu cha THAMANI hivyo
waithamini.
Lengo kuu la ujio wao pia lilikuwa kuwawezesha
Fikra Kubwa kuwa na ile dhamira ya dhati ya kuyapigania malengo yao na
kuyafikia bila kukwamia njiani, pamoja na hayo pia wanaFikra Kubwa kupata Fursa
ya kujua historia yao kuwa
·
Anaongea
na nani?
·
Alitoka
wapi?
·
Sasa
hivi yuko wapi?
·
Na
aliwezaje kufika alipo?
·
Changamoto
alizopitia na namna alivyozivuka
·
Na
kupewa ushauri kutoka kwao.
Hivyo
basi:
Wageni
wetu walipata nafasi ya kuzungumza na uongozi wa shule, na walimu wa kidato cha
nne na pili,wamewashukuru saana walimu kwa msaada mkubwa waliowapa mpaka hapo
walipofikia leo, Kutokana na majukumu mengine Mkuu wa shule alikaimu majukumu yake
aliyokusudiwa na kutarajiwa kwa makamu wa shule ambapo aliwatambulisha wageni
kwa FIKRA KUBWA na kupata fursa ya kila mgeni kuzungumza nao historia zao toka
walipojiunga Mabibo mpaka walipofikia leo. alasiri ilipofika walimaliza kuzungumza
na wanaFikra Kubwa kisha kumalizia na kuzungumza na wanafunzi wote wa kidato
cha pili na nne, na mwisho kunywa nao vinywaji mwalimu mlezi alivyotoa tuwape.
Ujio huu kwa wanafikra kubwa ni jambo
muhimu saana katika kujenga THAMANI ya Elimu ili waone umuhimu wa kusoma kwa
bidii wawe mfano wa kuigwa na wakumbukwe na shule na kutokuwa na sababu za
kufeli, hivyo baada ya watoa mada wote kuzungumza kwa nafasi yake kwa wanafikra
kubwa tulifanya tathmini kwa kuwasikia wanafikra kubwa baada ya mada
zilizowasilishwa walifurahi saana na pia wameshukuru saana ujio wao kwani
haukuwa wa bure, na wameogopa kufeli wakaahidi kujituma ili wafaulu zaidi yao.
Ni kweli wanafikra
kubwa wamejuzwa leo na wao kwa dhati kabisa wamejiridhisha kuwa hakuna sababu
ya wao kufeli kabisa.Kila mtoa mada aliwaeleza kuwa ili waweze kuyafikia
malengo yao ni lazima wajali
·
Muda
·
Wawe
na malengo,
·
Nidhamu
ya hali ya juu saana
·
Uthubutu
na kutokukata tama,
·
Wajifunze
kuwasaidia na wengine
·
Kuepuka
makundi rika na kuchagua marafiki wazuri.
·
Kuheshimu
walimu
·
Kusoma
kwa bidii siku zote n.k
RAI YANGU
Rai yangu kwa wataaluma wengine na
walezi shule nyingine ni kuwa watumieni wale Form IV waliomaliza katika shule
zenu miaka iliyopita na wakafaulu vizuri kwa kiwango cha Division II au I kama
wapo, kama hamna hata Division III sio mbaya, hawa wanafunzi wanajua mambo
mengi kuliko tujuavyo sisi, leo nimejifunza mambo mengi kupitia kwao na
nitayafanyia kazi.
Niwasihi wazazi/walezi wa wanafikra
kubwa leo wakifika nyumbani kila mmoja akueleze amejifunza nini kutoka kwa
wanafunzi walioalikwa leo shuleni, pia Umwambie mwanao mwaka huu asikubali
kushindwa kufaulu, ajitume zaidi kwa muda huu mfupi uliobaki.
WANAFIKRA
KUBWA TUNAAMINI WANAFUNZI WAZURI KITAALUMA HAWAZUKI TU, BALI HUANDALIWA.
Picha na
Matukio:
JAPHET E. MOSHI
MWALIMU MLEZI WA KUNDI( great
Thinkers)
Kwa mawasiliano zaidi ;
+255 714 781 432.
+255 755 558 159
Nakala kwa:
MLEZI NDOTO KUBWA
MwL Cleopa
E. Soi – AIONE
No comments:
Post a Comment