FIKRA
KUBWA GROUP (23)
KIDATO
CHA PILI – 2016
MABIBO
SEKONDARI
Na
Mwl Japhet E. Moshi
Ndugu
mzazi/mlezi na wadau wote wa Fikra Kubwa Group salaam.
Leo
wanafunzi wamemaliza mitihani yao ya Mock kidato cha pili, hivyo awamu ya
kwanza ya maandalizi imeisha kwa maana ya Mock na sasa tunaelekea kwenye
maandalizi makaubwa zaidi ya mtihani wa Taifa ambapo kuanzia kesho asubuhi
mikakati yetu inaendelea kama ifuatavyo;
1. Morning Prepo itaendelea
kesho asubuhi kuanzia saa 12:00 mpaka saa moja na nusu, na Evening Prepo
zitaendelea jioni kwa utaratibu wa awali mpaka saa 11:30 jioni. Hivyo kuanzia
kesho atachelewa kurudi nyumbani na mimi nitakuwa nao muda wote shuleni jioni.
2. Leo nimempa ratiba mpya ya
kujisomea binafsi kuanzia kesho mpaka mwishoni mwa mwezi wa kumi na somo moja
atalisoma kwa siku mbili kama ratiba yake inavyoonesha, Mzazi/mlezi msimamie
mwanao na hakikisha ratiba inafuatwa vizuri nyumbani na mwanafunzi anasoma muda
wote, kumbuka kupafanya nyumbani kuwe shule kwa ajili yake.
3. Siku ya jumatatu jioni
tutakuwa na DEBATE kati ya kundi la The Winners na Fikra Kubwa Motion inasem
“Are single SEX Schools more EFFECTIVE Than Co-ed Schools?”
mwambie ajiandae vizuri kwa ajili ya
motion hiyo ili aweze kuiwasilisha kwa wenzake wanaomtegemea ili kuleta ushindi
kwa group letu.
4. Jumamosi kutakuwa na mtihani wa somo
la BIOLOGY msihi asilaze damu katika hili, mwisho wa mtihani mmoja ndio mwanzo
wa mtihani mngine hivyo mtie moyo azidi kujituma kwa moyo wote katika masomo
yake. Kila wakati mkumbushe azingatie Mbinu 30 za kusoma ili kufaulu.
Mtihani wa taifa haupo
mbali hivyo jitihada za usimamizi zinahitajika ili mwanao aweze kufaulu kwa
kiwango tunachokitaka, Kumbuka mwanafunzi mzuri hazuki, bali huandaliwa.
Imeandaliwa na:
Mwl Japhet E.
Moshi
MLEZI FIKRA
KUBWA GROUP
Tembelea blogu
yetu
http://fikrakubwa.blogspot.com/
Na Ukurasa wetu
Facebook
KUJIFUNZA ZAIDI
No comments:
Post a Comment