Sunday, 4 September 2016

WAFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO WA SOKO LA MWENGE STAND (WAMANCHINGA) WACHANGIA VIFAA VYA ELIMU WILAYA YA KINONDONI.

WAFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO WA SOKO LA MWENGE STAND (WAMANCHINGA) WACHANGIA VIFAA VYA ELIMU WILAYA YA KINONDONI.

Na Mwl Japhet E. Moshi
Mlezi Fikra Kubwa Group.

🅾  Tarehe 6/08/2016 Nilialikwa niwe MC kwa hafla ya kukabidhi vifaa vya elimu hapa Mwenge stand ambapo Umoja wa wafanyabiashara ndogo ndogo wa Mwenge (WAMACHINGA) Wamekabidhi kwa Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi na Afisa Elimu K/ndoni Ndugu Rogers Shemwelekwa vifaa vya elimu ikiwemo madaftari Counter book na peni kwa watoto yatima, vifaa vyenye thamani ya Tshs 7,400,000/= kwa ajili ya wanafunzi 200 wa masikini wasiojiweza, wanaotoka katika familia masikini.
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Happ Salum, Mkurugenzi na Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni.

Hafla imekuwa nzuri sana kwani nijambo la kipekee kwa wamachinga kutoa mchango wao kuchangia Elimu. Ambapo wageni waliwapongeza wafanyabiashara hawa kwa juhudi hizi na kuwataka waendelee na juhudi hizi ili kuinua kiwango cha wasomi kwa kuwasaidia wadogo zao wapate vifaa vya elimu.
 Picha kushoto ni Afisa Elimu wetu wa Manispaa ya Kinondoni Ndugu Rogers Shemwelekwa, na kulia ni Mwl Japhet E. Moshi mlezi Fikra Kubwa group wakati wa kukabidhiwa vifaa vya elimu - Mwenge Stand.


Kwa pamoja Tukikabidhiwa vifaa mbalimbali vya elimu kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa Mwenge. (picha kulia ni Mwl Japhet E. MOSHI akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Kinondoni katikati)

Habari zaidi kwa yaliyojiri fuatailia habari kupitia vyombo vingine vya habari jioni ili uweze kuhabarika zaidi. Mungu ibariki Kinondonii. Mungu ibariki Tanzania.

picha na matukio zaidi





Mkuu wa wilaya mwisho aliondoka kwa bajaji.
Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
Mlezi Fikra Kubwa Group

No comments:

Post a Comment