Na Mwl Japhet E. Moshi
``mwanafunzi mzuri Kitaaluma hazuki tu, bali huandaliwa"
🅾 Leo katika kuwaandaa wanaFikra kubwa ili waweze kuwa na dhamira, ari, Kiu na nia ya dhati katika kuyafikia malengo yao tumewaalika wanafunzi wa shule ya udaktari (School of Medicine) mwaka wa 3 na wa 5 kutoka chuo kikuu cha Hurbert Kairuki University Ndugu Heaven E. Soi na Kelvin JUVENILE (MD) ili Wazungumze na wanafikra Kubwa wakiwajuza wao ni nani, wametoka wapi, na kwa sasa wapo wapi na wamefikaje hapo ili kuwapa hamasa na wao waweze kufika pale walipofika wao, na namna walivyozivuka changamoto mbali mbali mpaka kufanikiwa kufika Chuo Kikuu cha Hurbert Kairuki University ambapo leo wanasoma udaktari.
🅾 Heaven E Soi (MD) alipata fursa pia ya kuwafundisha wanafikra Kubwa thamani ya Elimu, na pia aliwasihi kamwe wasidharau mwanzo wao mdogo wa safari waliyoianzisha ili kufikia malengo yao, maana maisha ni hatua (Life is in stages) nayeye pia kabla hakufikia hapo alipo aliwahi kupita hapo walipo wao leo. Amewasihi wajali sana muda kwani kuna uhusiano mkubwa kati ya muda na mafanikio.
Picha Chini ni mwanafunzi wa udaktari mwaka wa tatu H. SOI akizungumza na wanafikra kubwa
- Ndugu KELVIN JUVENILE (MD) ambae anatarajia kugraduate mwisho wa mwezi huu wa nane, amewaeleza wanafunzi namna ya kusoma kwa bidii na kujali muda ili kufikia malengo yao hasa wale wenye ndoto za kuwa wanasayansi. Pia amewasihi kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa walimu/walezi/wazazi na wenzao ili waweze kufanikiwa.
Picha na matukio chini nia K. Juvenile MWANAFUNZI wa udaktari mwaka wa 5 akizungumza na wanafikra kubwa juu ya thamani ya elimu
Tulipata picha za pamoja
🅾 Baada ya mgeni kuondoka tumeendelea na Solving yetu kama kawaida ikiwa ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea mtihani wa Mock.
🅾 Morning na evening speech zimeendelea kama kawaida leo hivyo mzazi/mlezi endelea kumsihi mwanao aendelee kusoma kwa bidii kwani kesho wenzake wanamtegemea kwa ajili ya speech nzuri. Msimamie asome kwa kufuata ratiba yake ya mock.
Imeandaliwa na:
Mwl Japhet E. Moshi
Mlezi Fikra Kubwa Group.
Nakala kwa
Mwl Cleopa E Soi na wataaluma wote ~ waione
No comments:
Post a Comment