Wednesday, 31 August 2016

NAMNA MALEZI YA WALIMU KWA WANAFUNZI YANAVYOWEZA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU.

NAMNA MALEZI YA WALIMU KWA WANAFUNZI YANAVYOWEZA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAULU.

KATIKA KULEA WANAFUNZI TAMBUA CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI WAKO NA KUWASAIDIA KUZITATUA ILI WAWEZE KUFIKIA MALENGO YAO.

Unapolea wanafunzi tambua CHANGAMOTO zao wanazokutana nazo katika maisha na masomo, changamoto ambazo zinaweza kuwazuia kufikia ndoto zao na uzitatue, Hii itamsaidia mwanafunzi kufaulu vizuri.

~ Mimi nilipowatembelea wanafikra kubwa nyumbani kwao ili kutambua changamoto zilizopo shuleni na nyumbani zinazoweza mzuia mwanafikra kubwa asiweze kufikia ndoto zake, niliweza kubaini mmoja wa wanafunzi wangu nyumbani kwao hakuna umeme hivyo hawezi kusoma usiku kama ratiba niliyompangia inavyomuelekeza, baada ya kugundua changamoto hii nilimnunulia taa aina ya solar D LIGHT inayotumia mwanga wa jua ili imsaidie aweze kusoma vizuri wakati wa usiku.

Taa ile tulimkabidhi mwanafunzi huyu na alishukuru mno na kwa sasa anasoma vizuri wakati wa jioni kwani ile changamoto ya taa tuliitatua.


Hivyo nivizuri kwa mwalimu mlezi aweze kutambua changamoto za wanafunzi wake ili zisiwe kikwazo kwao kushindwa kufaulu mitihani yao.

Wanafunzi wengi wanachangamoto nyingi nyumbani na shuleni changamoto nyingi sana ambazo huwa kikwazo katika safari yao ya elimu, hivyo tusipozibaini hizo changamoto na kuzitatua mapema itakuwa nivigumu kwa mwanafunzi huyo kufaulu.

Imeandaliwa na:
MwL Japhet E Moshi
Mlezi Fikra Kubwa Group (23)
Mabibo Sekondari

HATUA 10 ZA KUANZA KULEA WANAFUNZI ILI WAWEZE KUFAULU

HATUA 10 ZA KUANZA KULEA WANAFUNZI ILI WAWEZE KUFAULU

1. Ufanyike mgawanyo sawa wa wanafunzi wa kidato cha pili na nne kwa walimu wote waliopo shule ili kufanya kwa ukaribu ufuatiliaji wa maendeleo ya kitaaluma, na nidhamu za wanafunzi na kuwa mshauri wa mwanafunzi husika na kumjulisha mkuu wa shule au mwalimu mwandamizi wa taaluma juu ya mwenendo na maendeleo ya mwanafunzi. (mfano wnafunzi wa kidato cha nne wako 200 na shule ina walimu 40, ina maana kila mwalimu atalea wanafunzi 5.
rejea Mkakati #7)

2. Kuwajua na kuwafahamu wanafunzi wako unaowalea.
- Ifahamu Historia ya kila mwanafunzi vizuri shuleni na nyumbani.
- Zifahamu Changamoto anazopitia kielimu na msaidie azivuke.
- Tembelea nyumbani kwake ili kumfahamu zaidi na kuonana na mzazi kujenga conection nzuri ya kumsimamia mwanae na mwombe aridhie kusimamamia ratiba ya kusoma ya mwanae anaporudi nyumbani..

3. Pata mawasiliano ya wazazi au walezi wake.
- Tengeneza network nzuri kati yako na wazazi kimawasiliano muda wote kwa njia ya message na ikiwezekana mpigie simu.
- Tengeneza kundi la whatsup la wazazi na walezi na wadau wa kundi lako ili kuweza kurahisisha mawasiliano ya matukio yote yanayoendelea kwa mwanae kila siku kwa muda wa ziada shuleni, na picha watumie waone.

4. Tengeneza jina la Group lako.
- Jina mtakalolichagua na wanafunzi wako liakisi ndoto zao na mission ya group
- Mfano Mabibo kuna magroup kama Fikra Kubwa, The winners, New Direction, Tumaini Jipya, Good Hope, 4G, Fikra Chanya n.k lakini Ukienda Gogoni kwa Mwl SOI wao wana NDOTO KUBWA na Yes I can. Kule Bunju kwa Mwalimu Safina wapo MAKONDA THE WINNERS na Maramba mawili utawakuta The white Horse.

5. Wafundishe wanafunzi wako thamani ya elimu.
- Elimu ni ya thamani kuliko kitu kingine chochote katika taifa hili, toa mfano wa kazi mbali mbali, mfano kulima na kusoma ipi ni kazi ngumu n.k
Raisi wa Africa kusini Hayati Nelsoni Mandela alipata kusema kuwa
“Elimu iliyojitosheleza ni INJINI KUBWA ya maendeleo, lakini elimu isiyojitosheleza ni Umasikini Mkubwa”
“Ni kupitia Elimu ambapo mtoto wa mkulima masikini anaweza kuwa Daktari mkubwa sana, na ni kupitia Elimu ambapo mtoto wa kibarua wa mgodini anaweza kuja kumiliki mgodi mkubwa wa Dhahabu, na ni kupitia Elimu hiyo hiyo ambapo mtoto wa kibarua wa shambani anaweza kuja kuwa raisi mkubwa wa nchi”
-Tafuta watu wa kuzungumza nao kwa kuanza na wale waliomaliza hapo shuleni waje wawasaidie wenzao wasikwame, wawaeleze wenzao namna walivyozivuka changamoto.
- Andaa study tour nia ni kujenga hamasa zaidi ya wao kutaka kusoma ili wafaulu.
- watafutie wataalamu waliowatangulia wawafundishe hatua walizopitia hadi wakafika walipo, Mfano: kuna anayetaka kuwa profesa, mtafute Profesa amuelekeze, Daktari mtafutie daktari atampa mwangaza zaidi n.k ili wakusaidie kukufundishia thamani ya elimu.




6. Wapangie kila mmoja ratiba yake ziwe ratiba mbili.
Wapangie ratiba ya matukio ya kila siku nyumbani na ratiba ya kusoma nyumbani izingatie masomo yake ya shule siku inayofuata. Ratiba hizi zibandikwe nyumbani mwanafunzi anaposomea na lazima awe na SAA YA MKONONI. Ni vema akiwa anasoma awe na SAA, hii itamsaidia kuelewa muda halisi aliosoma.





7. Wafundishe Mbinu za kufaulu na Kanuni za msingi za kuwasaidia kusoma wafaulu.
(zingatia Mbinu 30 za kufaulu mtihani toka Fikra kubwa Group)

8. Tengeneza mpango kazi na mkakati wa kundi wa siku, wiki, mwezi na miezi kadhaa.
- Siku za kuwasilisha mada kwa manafunzi mmoja mmoja.
- Siku za group discussion
- Siku watafanya test/mitihani.
- Siku watakuwa na study tour n.k

9. Usimamizi na Tathmini ( Monitoring and evaluation)
- Kama kundi halitasimamiwa vizuri, halitaweza kufanya vizuri, usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa kundi ni muhimu saana ili kupata matokeo mazuri ya kundi lako.



10. Chagua viongozi wa kuliongoza kundi wakati haupo, mathalani mwenyekiti na katibu wa kundi.
“Fikra Kubwa Tunaamini mwanafunzi mzuri kitaaluma hazuki tu, bali huandaliwa”.




Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
MLEZI FIKRA KUBWA GROUP.

http://fikrakubwa.blogspot.com/


https://www.facebook.com/groups/1730512107203946/

Nakala kwa
Mwl Cleopa E. SOi na walezi wote waione.

IFAHAMU MIKAKATI 11 YA KUONGEZA UFAULU IDARA YA ELIMU - WILAYA YA KINONDONI.

IFAHAMU MIKAKATI 11 YA KUONGEZA UFAULU IDARA YA ELIMU - WILAYA YA KINONDONI.

Mikakati hii 11 ni mikakati ya Manispaa ya Kinondoni ya idara ya elimu ya Kuongeza ufaulu wa Kidato cha pili na kidato cha nne, mikakati hii ya idara ya elimu ilianzishwa na Afisa Elimu wetu Ndugu ROGERS SHEMWELEKWA na tuliiafiki kwa pamoja na ilipitishwa na kikao cha wakuu wa shule zote na walimu wa Taaluma mwaka jana 2015. Malezi tunayoyafanya leo hii kupitia makundi mbalimbali mashuleni kwetu ni zao la Mkakati Na. 7 kati ya 11 wa Manispaaa ya Kinondoni idara ya Elimu.

MIKAKATI 11 YA KUONGEZA UFAULU WA KIDATO CHA PILI NA NNE ILIYOPITISHWA NA KIKAO CHA WAKUU WA SHULE, WALIMU WA TAALUMA NA IDARA YA ELIMU WILAYA YA KINONDONI

1. Madarasa ya Mtihani yaani kidato cha Pili na Nne kila siku asubuhi wafanye mazoezi ya asubuhi (morning test) kwa topiki 2 kwa kila somo kwa kuanza na “syllabus” ya kidato cha I, ije cha Pili, Tatu na Hatimae kidato cha nne.

2. Mada ambazo watakuwa wanafunzi wamefanya vibaya kwa majaribio ya asubuhi, zirudiwe kufundishwa ili kujenga uelewa mzuri wa mada kwa wanafunzi.

3. Kila mwezi kufanyike majaribio ya mwezi kwa kuwa mwezi una wiki 4, kila wiki kufanyike majaribio ya Masomo 2 (Monthly Test) mwezi ukiisha masomo 8 ya Msingi yatakuwa yamefikiwa. Aidha kwa yale masomo mengine (Optional Subject) Majaribio yafanyike siku za ijumaa. Wajumbe waliazimia majaribio ya mwezi yafanyike kwa siku za jumamosi.

4. Maswali yanayotungwa yawe kwenye mfumo wa Baraza la mtihani la taifa (NECTA) ili kuwaandaa vema wanafunzi na mitihani ya taifa.

5. Kila mwanafunzi awe na daftari 2 za kila somo, Daftari la nukuu za somo (Lesson Notes) na daftari la Mazoezi ya somo hilo.

6. Ratiba ya mazoezi ya asubuhi (Morning Test) na majaribio ya mwezi (Monthly Test) ibandikwe kwenye mbao za matangazo za shule. Wazazi wa kutwa wajulishwe na walimu washirikishwe kikamilifu.

7. Ufanyike mgawanyo sawa wa wanafunzi wa kidato cha pili na nne kwa walimu wote waliopo shule ili kufanya kwa ukaribu ufuatiliaji wa maendeleo ya kitaaluma, na nidhamu za wanafunzi na kuwa mshauri wa mwanafunzi husika na kumjulisha mkuu wa shule au mwalimu mwandamizi wa taaluma juu ya mwenendo na maendeleo ya mwanafunzi. (mfano wnafunzi wa kidato cha nne wako 200 na shule ina walimu 40, ina maana kila mwalimu atalea wanafunzi 5.

8. Kufanyike ufuatiliaji wa karibu wa Nidhamu za wanafunzi na mienendo yao. Aidha walimu tuendelee kuwa wazazi na walezi bora wa wanafunzi kimaadili na kinidhamu.

9. Kila siku kuwe na ripoti ya ufundishaji na taarifa itolewe kwa mkuu wa shule. Aidha kila ijumaa kufanyike kikao cha Taaluma ambacho Mwenyekiti wake amependekezwa jkuwa Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma na Katibu Mwallimuu wa Zamu kwa wiki husika. Kwa shule zenye Makamu wa wakuu wa shule Taaluma, hawa wawe wenyeviti na katibu awe Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma. Wajumbe wawe wakuu wote wa idara za Masomo. Taarifa ya ufundishaji ya wiki iwasilishwe kwa Mkuu wa Shule.

10. Kila siku ya ijumaa Mkuu wa shule apitie taarifa zote za ufundishaji yaani class Journals, Lesson Plan, Record Keeping book (Daftari linalotunza alama za wanafunzi za mazoezi na majaribio), Subject Log book na daftari za mazoezi ya wanafunzi. Pia Mkuu wa shule afuatilie nukuu za somo zinazotolewa kwa wanafunzi (lesson Notes).

11. Mwalimu Mwandamizi wa Taaluma apunguziwe vipindi ili aweze kufanya ufuatiliaji wa ufundishaji wa walimu na kila au kabla ya tarehe 05 ya kila mwezi walimu wote wafanye kikao kupitia ufundishaji wa mwezi husika. Mwenyekiti atakuwa Mkuu wa Shule na Katibu atakuwa Mwalimu Mwandamizi Taaluma. Mukthtasari wa kikao hicho utawasilishwa kwa Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa. Ni vizuri kupitia ufundishaji wa kila somo, mazoezi ya kila siku yaliyotolewa, majaribio na hali ya ufundishaji. Aidha kikao kiliamua mada kwa madarasa ya mtihani ziwe zimekwisha kabla ya mwezi Julai, 2015.

Hii ndio mikakati 11 ya kuongeza ufaulu na ni kupitia mikakati hii ambapo Mkakati Na 7 na Na. 8 wa Malezi umetupa fursa hii ya kuwa na Makundi mbali mbali ili kufuatilia kwa ukaribu maendeleo yao kitaaluma.

WITO
Wito wangu kwa walimu nchini karibuni sana Kinondoni Manispaa IDARA YA Elimu Sekondari, Karibuni Fikra Kubwa Group Mabibo mje kujifunza, na shule kama Gogoni, Bunju , Maramba Mawili mjifunze kuongeza kiwango cha ufaulu kupitia malezi kwa wanafunzi wetu.

Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
MLEZI FIKRA KUBWA GROUP.

http://fikrakubwa.blogspot.com/

https://www.facebook.com/groups/1730512107203946/

Nakala kwa
Mwl Cleopa E. SOi na walezi wote waione.

KWANINI MWALIMU AWE MLEZI KITAALUMA?

KWANINI MWALIMU AWE MLEZI KITAALUMA?

SABABU:

1.Tunalea ili ufanyike ufuatiliaji wa karibu wa Nidhamu za wanafunzi na mienendo yao. Aidha walimu tuendelee kuwa wazazi na walezi bora wa wanafunzi kimaadili na kinidhamu ili kuongeza ufaulu.

2. Ni jukumu letu kama walimu tukisaidiana na mzazi kumwandaa mwanafunzi mzuri kitaaluma. (Fikra Kubwa Tunaamini kuwa Mwanafunzi mzuri kitaaluma hazuki tu, bali huandaliwa). Hili jukumu la kumwandaa mwanafunzi mzuri kitaaluma serikali imekuamini ikakupa wewe mwalimu, lifanye kwa moyo wote bila kuangalia changamoto zinazokuzunguka kila kona.

3. Kumbuka Sisi tulilelewa ndio maana tupo hivi tulivyo, hata nguo, viatu, magari, meza n.k unavyoviona kuna mtu alilelewa akafikia umri wa kuweza kutengeneza unachokiona leo. Hivyo hatuna budi kuhakikisha na sisi tunalea wanafunzi ili kuandaa madaktari, walimu na wataalamu wengi zaidi kwa miaka inayokuja.

4. Takwimu za ufaulu kitaifa na katika shule zetu sio nzuri kabisa, sisi wenyewe ni mashahidi wa kwanza, ukiangalia wanafunzi wanaosajiliwa kwa ajili ya mtihani wa taifa katika shule zetu , na ukiangalia idadi ya wale waliochaguliwa kwenda kidato cha tano baada ya matokeo kutoka utagundua dhahiri shairi kuwa takwimu sio nzuri kabisa. Wanaosajiliwa ni wengi lakini wanaofaulu ni wacahche mno, hivyo inahitajika mwalimu afanye zaidi ya jukumu lake la kufundisha ili kubadili hizi takwimu mbaya za ufaulu.

5. Mwalimu aliwahi kuwa mwanafunzi; hivyo mwalimu anaelewa namna gani ya kumfundisha mwanafunzi ili afaulu kwani mwalimu yeye hakufeli. Kama mwalimu hakufeli akiamua kumsaidia mwanafunzi kwa Moyo wa dhati huyo mwanafunzi hawezi kufeli.

Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
MLEZI FIKRA KUBWA GROUP.

http://fikrakubwa.blogspot.com/


https://www.facebook.com/groups/1730512107203946/

Nakala kwa
Mwl Cleopa E. SOi na walezi wote waione







 walezi wa wanafunzi tukiwa pamoja na wanafunzi tunaowalea kitaaluma

HISTORIA YA KUNDI LA FIKRA KUBWA NA SAFARI YA KUTEMBELEA CHUO KIKUU CHA MUHAS

HISTORIA YA KUNDI LA FIKRA KUBWA NA SAFARI YA KUTEMBELEA CHUO KIKUU CHA MUHAS

Fikra kubwa / great thinkers ni kikundi cha Wanafunzi 23 kwa sasa wenye ndoto za kuwa madaktari bingwa cha Mabibo Sec zao la Mkakati Na. 07 wa Manispaa ya Kinondoni kati ya Mikakati 11 ya Idara ya Elimu iliyoanzishwa na Afisa Elimu wetu Rogers Shemwelekwa tuliyoafiki Wakuu wa Shule, Wataaluma na Walimu kuwagawa wanafunzi ktk vikundi na kuvipa majina ya kitaaluma ambapo walimu wanapata fursa ya Malezi hasa Madarasa ya Mtihani.

Shule yetu ya Mabibo ikiongozwa na mkuu wetu Haki Mwasomola tuna vikundi vingi baadhi Tumaini jipya, New Direction, Fikra chanya,nk
Gogoni sec kwa MwL Cleopa Soi kuna Ndoto kubwa na Yes I can na Bunju sec kwa mwalimu Safina kuna Makonda The Winners ndio maana nasema ni mkakati wa Afisa Elimu wetu Rogers Shemwelekwa kuongeza ufaulu.

1. Mkakati wa Malezi ndio umetupa fursa hii ya kuwa chuo adimu kwa ajili ya Wanasayansi hawa wa fikra kubwa kuona ninako watazamia kesho wawepo.

2. Naamini wao kuona na kuwaona wanachuo waliosoma tena nyakati ngumu elimu sio bure kama sasa na mazingira ya kiwa magumu na bado wakafaulu itawaongezea hamasa ya kusoma kufikia ndoto zao za kuwa madaktari.

3.Katika malezi ya fikra kubwa tunafundisha fikra za kesho yao elimu ni injini kubwa ya maendeleo yao na jamii, tunawaandaa kumiliki na kutawala kwa njia ya elimu, tunawafundisha thamani ya kupenda elimu kuliko chochote, kujitambua, kuokoa muda, kuwaonyesha thamani ya elimu.

4.Wito kwa walimu nchini karibuni Kinondoni Manispaa idara ya elimu Karibuni mabibo mjifunze na shule kama Gogoni, Makumbusho, Bunju mjifunze kuongeza kiwango cha ufaulu kwa malezi.

5.Nipongeze jitihada za Rais, Waziri wa Elimu na wadau kuona Sayansi ni masomo ya Lazima kidato cha I -IV itasaidia Wanafunzi kuwa kama wapendavyo kama hawa wa fikra kubwa ambao usiku na mchana naomba Mungu anisaidie nichangie sehemu kama mwalimu wawe Madaktari wataalamubingwa kama jinsi chuo hiki watawasikia wa fani yao na kuwaona kaka na dada zao na zaidi chuo kikuu cha afya na tiba Muhimbili.

6.Tunaishukuru Serikali kuendeleza kutatua changamoto za walimu wa sayansi, maabara, chemical na vitabu visififishe ndoto zao za kuwa madaktari kwani elimu isiyojitosheleza ni umaskini zaidi wakati inayojitosheleza kama kutoishia kidato cha nne hadi ufike chuo kupata shahada, uzamili, uzamivu, Prof ni injini kubwa ya maendeleo.

Wenzetu India waziri wao mkuu alitembelea Tanzania wenzetu kati ya wanachojivunia na tunu kwao ni kuwa Taifa la wanasayansi
HAYATI NELSON MANDELA alikuwa Rais wa Afrika kusini alipata kunena, "Elimu ni silaha ya kuitawala dunia"

Mwalimu akasema ili tuendelee tunahitaji pia kupambana na adui ujinga
Sisi fikra kubwa tunaamini tunaweza kuwa madaktari kwa kubadilika tunavyofikiri tumetembelea chuo hiki tufikiri kichuo ili wajitume zaidi.

Ikumbukwe mwanafunzi mzuri kitaaluma na mtaalamu mzuri hazuki tu, bali huandaliwa.

Imeandaliwa na
Mwl JAPHET E. MOSHI
MLEZI FIKRA KUBWA GROUP
MABIBO SEKONDARI





WAZAZI NA WAALIMU NDIO MSINGI BORA WA MALEZI YA WATOTO PINDI WANAPOKUWA SHULENI.


WAZAZI NA WAALIMU NDIO MSINGI BORA WA MALEZI YA WATOTO PINDI WANAPOKUWA SHULENI.

MALEZI ni uangalizi Wa karibu Wa wazazi Kwa watoto wake ki Imani,kiafya,kiakili,kitabia,pia tukumbuke kuwa mungu ndiye muanzilishi Wa watoto. Mungu alipo muumba Adam,akamfanyia msaidiz wake Hawa akasema zaeni mkaongezeke. Hivyo malezi bora ni jambo la kuzingatia Kwa watoto wetu Kwa wazazi wote kushirikiana.
Hivi sasa hali imekuwa tofauti sana unakuta mama na baba wanakuwa mbali na watoto wao hata kama wanaishi Nyumba moja jambo linalopelekea watoto kukosa malezi bora na kupelekea watoto kutakuwa watiifu,waadilifu,na kupelekea kutokuwa waaminifu na kusababisha watoto kushuka kitaaluma kama wanasoma chanzo cha ayo yote ni kutokuwa na malezi bora kutoka Kwa wazazi na ufuatiliaji Wa karibu Kwa watoto wao.


Pia tunaona baadhi ya wazazi wanaamua kuwapeleka watoto wao kusoma katika shule za bweni zilizo mbali na wanapoishi Kwa kisingizio cha kukwepa bughudha au usumbufu Wa watoto pindi wanapokuwa nyumbani na kujikuta Wa kikwepa majukum ya malezi Kwa watoto wao.
Upande Wa pili Kwa kuwa wanafunzi ni wengi WAALIMU wanashindwa kuwamudu,kuwahudumia watoto Kwa wingi wao na kupelekea kukosekana Kwa ukaribu unaotakiwa na kufanya watoto "kujiokotea"tabia za kuiga mambo mengi mabaya ambayo ni hatari Kwa maisha yake ya baadae.
Watoto pindi wanapokuwa masomoni ni wajibu Wa WAZAZI kushirikiana na WAALIMU Kwa ukaribu kufuatilia Kwa karibu maendeleo ya darasani Kwa maana Kuwachunguza kitabia,ufuatiliaji Wa mazoezi wanayopewa shule kama wanafanya n.k
Na pindi ugunduapo dosar zozote zile Ina kuwa rahisi Kwa MZAZI kuziona na kutoa msaada,mawasiliano kati ya WAZAZI na WAALIMU yawe ya Mara Kwa Mara Kwa maana ya wazazi kuwatembelea watoto shuleni wanakosoma na Wala siokusubilia Siku ya kufuata ripot za matokeo ya mitian ya watoto wao au kwenye vikao vya wazazi pindi wanapoitajika mashuleni na kutaka kujua mienendo ya watoto wao pindi wanapo kuwa shuleni
Hivyo basi tunaona MAWASILIANO ni muhimu sana kati ya WAZAZI na WAALIMU katika kufaham maendeleo ya wanafunzi kitaaluma na kitabia ni vyema wazazi wawe Karibu na watoto wao ili waweze kuwa jenga kimaadili,kitaaluma,kiafya ili wawe wamekuwa katika misingi bora ya malezi ya WAZAZI na WAALIMU waje kujenga taifa letu.
By
JUMANNE ABDUL


ZIARA YA AFISA ELIMU WA MANISPAA YA KINONDONI BUNJU SEKONDARI

ZIARA YA AFISA ELIMU WA MANISPAA YA KINONDONI.

Afisa Elimu Ndugu Rogers Shemwelekwa alipowatembelea wanakambi wa Bunju sekondari wanaojulikana kwa jina la MAKONDA THE WINNERS.
Huu ni moja wapo ya mkakati 11 ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa Manispaa ya Kinondoni ambapo Bunju sekondari kwa Mwalimu Safina amewaweka wanafunzi wake kwenye kambi moja ili waweze kujiandaa vizuri waweze kufaulu katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye mitihani.
Afisa Elimu wetu ndugu Rogers Shemwelekwa mwasisi wa mikakati hii akiongozana na Familia yake walitembelea MAKONDA THE WINNERS na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mchele na vyakula watakavyokula pindi wawapo kambini wakijiandaa na mtihani wao wa taifa.

Wanafunzi wa kidato cha pili wa Bunju Sekondari Kikundi cha MAKONDA THE WINNERS wanafunzi anaowalea Mwalimu Safina wakiwa pamoja na Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni Ndugu Rogers Shemwelekwa alipowatembelea na familia yake.

Tuesday, 30 August 2016

HERI KWA WANAFUNZI WA WAFIKRA KUBWA GROUP.

HERI KWA WANAFUNZI WA WAFIKRA KUBWA GROUP.


NAUTOA UKUTA HUU LEO KWA WANAFIKRA KUBWA GROUP.
NAWATAKIA WANAFIKRA KUBWA KILA LA KHERI KATIKA MITIHANI YAO YA MOCK KIDATO CHA PILI INAYOANZA LEO.



Kutembelewa na madacktari bingwa kutoka Muhimbili

FIKRA KUBWA GROUP KIDATO CHA PILI 2016 MABIBO SEKONDARI

Na Mwl Japhet E. Moshi

Tumekuwa na ugeni leo kutoka chuo kikuu cha Muhimbili MUHAS ukiongozwa na
Dr. Albert ~ Mhadhiri MUHAS na daktari wa Kinga Muhimbili.
Dr Isaac Maro ~ Daktari Muhimbili na mwanafunzi wa PHD anayoisomea TOKYO JAPAN.
Dr Isaac Maro pia ni mtangazaji na host wa kipindi cha Njia panda clouds radio kila jumapili.
Dr Isaac maro na Albert waliongozana na madaktari wenzao wawili kutoka Japan ambao ni Dr Sapto na Dr Bumpei ambao walikuja na kuwatembelea Fikra kubwa baada ya kuwaona juzi Muhimbili tulipowatembelea na tukawaomba waje kuwainspire Fikra kubwa Group.
Kila mmoja alipata nafasi ya kuzungumza na Fikra Kubwa juu ya thamani ya Elimu na namna ya kuweza kuyafikia malengo yao makubwa waliyokuwa nayo. Baada ya kuzungumza na Fikra Kubwa walipata fursa pia ya kuzungumza na shule nzima na kuwasihi wapende kuukomboa wakati kwani muda ukipita haurudi tena.


READ MORE AT........
Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
Mlezi Fikra Kubwa Group
Nakala kwa
Mwl Cleopa E Soi na walezi wote waione.

Zifahamu Mbinu 30 za kufaulu mitihani

FIKRA KUBWA GROUP KIDATO CHA PILI 206 MABIBO SEKONDARI
Na Mwl Japhet E. Moshi


Leo nimewafundisha wanafikra kubwa Mbinu 30 za kufaulu ili wazitumie tunapoelekea kwenye Mock na Taifa.
 Kila mmoja nimempa nakala ya mbinu hizi ili zimsaidie katika maandalizi ili wafaulu. Baada ya kuwapa nakala tulifanya maombi /dua kuliombea kundi kwa ajili ya mitihani iliyo mbele yetu.
MBINU 30 ZA KUFAULU KATIKA MASOMO
1. Jenga tabia ya kuyaombea masomo yako kila siku na kila mara, wanafunzi wengi waliofaulu walimweka Mungu mbele kwenye masomo yao.
2. Yapende masomo yako na tena uyafurahie.
3. Ni vema ukiwa unasoma uwe na SAA, hii itakusaidia kuelewa muda halisi uliosoma.
4. Hakikisha unapoanza kusoma uwe umekaa mahali ambapo pana utulivu na hupati usumbufu usio na sababu za msingi.
5. Kabla ya kuanza kusoma hakikisha, una kila kitu unachohitaji wakati wa kusoma mfano vitabu, kalamu, karatasi n.k
6. Wakati wa kusoma hakikisha unakuwa na daftari jingine ambalo utakuwa unaandika mambo usiyoyafahamu vizuri.
7. Kuwa na ratiba yako binafsi inayohusu masomo na uhakikishe unaifuata.
8. Tambua ni njia gani ukisoma unaelewa zaidi na ni wakati gani?. Je unaelewa zaidi asubuhi, mchana, jioni, usiku, baada ya kula, kabla ya kuoga, baada ya kufurahi,mitihani inapokaribia n.k
9. Epuka makundi mabaya ya wanafunzi wenzio wasiopenda kusoma na watu wanaopenda utani au mizaha, kutojali kuliko kilichowapeleka shule.
10. Kuwa na marafiki ambao mtakuwa mmejenga utararatibu wa kuulizana au kuandikiana maswali, kutokana na kile mlichojifunza.
11. Ili ufaulu ni lazima uwe na bidii sana katika kusoma, na epuka uvivu.
12. Sahau matokeo mabaya uliyoyapata katika mitihani iliyopita
13. Ukishasoma, hakikisha unapata mapumziko ya kutosha.
14. Kula ni kitu muhimu, hivyo hakikisha umeshiba na sio vema mara umalizapo kula ukaanza kusoma, mimi kama mwalimu wa biology nakushauri pumzika kidogo na jenga tabia ya kunywa maji mengi, mboga za majani na matunda kwa wingi.
15. Jenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili kama vile kucheza mpira, au kuruka kamba n.k
16. Tafuta kwa bidii, kujua sababu za wewe kufeli.
17. Kaa na wale wanaoweza kile usichokiweza.
18. Uliza waliokutangulia hatua walizopitia hadi wakafika walipo, Mfano: unataka kuwa profesa, mtafute Profesa akuelekeze, Daktari mtafute daktari atakupa mwangaza zaidi n.k
19. Waheshimu sana wale wote wanaokulea na kukuhudumia kama mwanafunzi.
20. Kubali kurekebishwa na kusahihishwa pale unapokosea.
21. Ombea mitihani yako kila siku, mpaka umerudishiwa majibu/matokeo yako
22. Kumbuka kuwaombea wasahihishaji. Na wao pia ni watu wanachoka na kukosea
23. Usifurahi kufeli kwa mwenzako.
24. Acha tabia ya kuchagua vipindi vya kuhudhuria darasani wakati masomo yote unatakiwa kuyafanyia mtihani.
25. Msikilize mwalimu vizuri anapokuwa anafundisha darasani utafaulu
26. Soma maelekezo ya mtihani (instructions) kwa makini
27. Usijibu swali bila kuelewa linataka nini?jibu utakalojibu litakuwa tofauti na swali. Hivyo soma swali zaidi ya mara moja ili ulielewe vizuri kabla ya kulijibu.
28. Usiwe na haraka ya kumaliza mtihani kwani kutakufanya usijibu kwa umakini.
29. Usiendekeze usingizi katika muda wako wa kujisomea.
30. Hakikisha haukati TAMAA.
mzazi msimamie mwanao aendelee kusoma kwa bidii kwani mtihani unaanza J3.
Imeandaliwa na
Japhet E Moshi
Mlezi Fikra Kubwa
Nakala kwa
Mwl Cleopa E Soi na walezi wote waione.

Debate na Evening prepo kwa wana FIKRA KUBWA GROUP

FIKRA KUBWA GROUP (23)
KIDATO CHA PILI 2016
MABIBO SEKONDARI




 Leo tumefanya debate na evening prepo vizuri jioni, muda wa kuchangia mada umekuwa mdogo na wanafikra Kubwa wameomba mjadala uendelee na kesho pia na nimewaahidi kesho jioni tutaendelea na Mada kwani imewavuta wengi mno waliotamani kushiriki, mpaka wasiokuwa kwenye makundi yetu waliomba kuja kushiriki.
Nilichojifunza leo ni kuwa debate ni nzuri mno na zinawafanya wanafunzi wajifunze kiingereza kwa lazima ili waweze kuchangia mada, nimeona hata wasiojiweza kiingereza wakifanya vizuri mno.
Kesho mada ni ile ile
``Girls themselves are the source of early Pregnancy"

Rai yangu kwa walezi wenzangu ni kuwa debate zina vitu vingi vya kujifunza toka kwa wanafunzi, hivyo mkipata muda waandalieni Mada mtajifunza mengi ya kuwasaidia. Leo mimi nimejifunza na nimeona iko haja ya mjadala uendelee na kesho ili nijifunze zaidi.
Kesho asubuhi Morning prepo itaendelea kama kawaida, hivyo mzazi mkumbushe mwanao kuwahi kama leo alivyowahi.


Imeandaliwa na
Mwl Japhet E. Moshi
Mlezi Fikra Kubwa Group
Nakala kwa
Mwl Cleopa E. Soi
Mlezi ndoto kubwa na wataaluma wote ~ waione

Wazazi kutembelea Fikra Kubwa Group

Wazazi kutembelea Fikra Kubwa Group


wanafikra Kubwa asubuhi hii tukiwa Morning Prepo tumetembelewa na mzazi mmoja wa Fikra Kubwa Group (MAMA BAKARI KISUA), baada ya kusikia jitihada hizi anasema ameguswa sana na ikabidi kuamkia hapa ili kuwatia Moyo, tumeongea mengi na nimejifunza vingi mno kwa dakika chache nilizokaa nae. Mungu akubariki mno mama kwa kukubali kuwa sehemu ya msaada kitaaluma juu ya wanafikra kubwa
Mzazi alipata fursa pia ya kuwaona wanaFikra Kubwa asubuhi hii waiendelea na Morning Prepo na amewatia Moyo wazidi kupambana na elimu bila Kumsahau Mungu wakati wote.
Nimebarikiwa sana kwa ujio wako. MUNGU aendelee kuwapigania namm nazidi kuendelea kuwa na nguvu katika kuwajengea wanafikra kubwa uwezo mkubwa kitaaluma